Polisi Kigoma imemtia mbaroni mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Shaban (21) Mkazi wa Buronge Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwamba ametekwa (Alijiteka) ili kuwezesha wazazi wake kutoa fedha kwa watekaji aweze kukombolewa na kua huru.
Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Filemon Makungu alieleza hayo akito taarifa kwa @ayotv_ mjini Kigoma alibainisha kuwa anayejulikana kwa jina Maarufu la Kocha ambapo Mei 14 mwaka huu mtu huyo alitoa taarifa kwa wazazi wake akidai ametekwa na watekaji wanadai kiasi cha shilingi milioni 2.5 ili waweze kumkomboa kwa hao watekaji.
Akiwa mafichoni ambapo alikua amejificha mtu huyo alikuwa akipiga simu kwa wazazi wake watoe fedha haraka ili waweze kumuachia kwani wakichelewa watekaji wanaweza kumuua kabisa,Kufuatia shinikizo hilo wazazi wa mtu huyo walitoa taarifa polisi ambapo upelelezi ulianza mara moja huku polisi wakiwasihi wazazi wa mtu huyo kutotuma fedha kwa mtu yeyote kuhusiana na tukio.
Kamanda wa polisi mkoa Kigoma alisema kuwa wakati polisi wakiendelea na upelelezi Ramadhani alifikishwa na wazazi wake kituo kikuu cha polisi mkoa Kigoma wakieleza kuwa amepatikana eneo la Msimba Dampo nje kidogo ya manispaa ya Kigoma Ujiji baada ya kutoa fedha kwa watekaji.
Hata hivyo polisi waligundua kuwa Mtuhumiwa huyo akiwa na washirika wake wawili Kassimu Kibona na Ramadhani Issa walitoa taarifa za uongo zilizoleta hofu na tahatuki ndani ya jamii kwa nia ya kujipatia fedha na hivyo kuwatia mbaroni ambapo wanatarajia kufikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.