Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini SACP David Misime leo June 12, 2020 ametoa taarifa juu ya uchunguzi waliofanya Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio la Freeman Mbowe kushambuliwa.
“Uchunguzi wetu umethibitisha kuwa siku ya tarehe 8/6/2020 Mhe. Mbowe alitembelea sehemu kadha za starehe zinazouza vileo ikiwepo Royal Village na kupata kinywaji. Hata alipofika hospitalini alionekana akiwa katika hali ya ulevi chakari kiasi cha kushindwa kutamka maneno sawa sawa” Misime