Polisi nchini Uganda imegundua mabomu matatu katika eneo la Lungujja mjini Kampala ikiwa ni saa chache tu baada ya kumtia mbaroni mtu mmoja baada ya kuingia kanisani katika mji mkuu wa Kampala akiwa na kilipuzi alichopanga kukitumia kufanya shambulizi.
Polisi ya Uganda imethibitisha kwamba, jana iligundua mabomu matatu katika nyumba moja huko Lungujja katika viunga vya mji mkuu Kampala.
Mtuhumiwa huyo ambaye ni mwanaume mwenye umri wa miaka 28 aliyetajwa kwa jina la Kintu Ibrahim, alikamatwa alipokuwa akikaribia kuingia katika kanisa la Pentekoste, Lubaga Miracle Centre, katika kitongoji cha Lubaga kusini mwa Kampala.
Maafisa wa polisi walikuwa wakiwatafuta wanaume wengine watatu pia wanaoaminika kutumwa kwenye mipango kama hiyo ya ulipuaji wa mabomu kwingineko nchini Uganda, imesema taarifa ya polisi ya Uganda.
Polisi ya Uganda imetoa taarifa ikitanabahisha juu ya kuweko njama za kutekelezwa mashambulio ya kigaidi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki