Kutumwa kwa maafisa wa polisi wa kwanza wa Kenya kwenda Haiti kuongoza kikosi cha kimataifa cha kupambana na genge kumecheleweshwa baada ya safari ya ndege iliyokuwa imepangwa kutoka Nairobi kuahirishwa siku ya Jumanne, vyanzo viwili vilivyoarifiwa kuhusu suala hilo vililiambia Reuters.
Maafisa wa Marekani hapo awali walikuwa wamedokeza kwamba maafisa hao watakuwa Port-au-Prince kufikia Alhamisi ili sanjari na ziara ya kitaifa ya Rais wa Kenya William Ruto katika Ikulu ya White House.
Akizungumza katika mkutano wa pamoja wa wanahabari na Rais wa Marekani Joe Biden, Ruto alikariri kujitolea kwa Kenya kuwatuma maafisa hao nchini Haiti.
Kenya ilijitolea mwezi Julai kuongoza ujumbe huo lakini imekuwa ikikabiliwa na ucheleweshaji wa mara kwa mara wa kutumwa kazini kutokana na kesi zilizoletwa na wapinzani wa mpango wa serikali na kuongezeka kwa ghasia mwezi Machi na kusababisha waziri mkuu wa Haiti kujiuzulu.