Polisi wa Uingereza walifanya ukaguzi katioka bustani kubwa ya London siku ya Ijumaa kumtafuta mwanajeshi wa zamani ambaye alitoroka gerezani akisubiri kufunguliwa mashtaka kwa tuhuma za ugaidi.
Polisi wa Metropolitan walithibitisha kuwa msako wa Richmond Park ulioko kusini-magharibi mwa jiji hilo, ambao ulihusisha helikopta mbili na maafisa waliokuwa chini, uliunganishwa kwenye msako wa Daniel Abed Khalife.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 aliteleza kutoka katika Gereza la Wandsworth Jumatano asubuhi alipokuwa akifanya kazi jikoni, inaonekana kwa kung’ang’ania chini ya lori la kupeleka chakula, polisi walisema.
Khalife anatuhumiwa kwa kutega mabomu bandia katika kambi ya kijeshi na kukiuka Sheria ya Siri Rasmi ya Uingereza kwa kukusanya taarifa “ambazo zinaweza kuwa na manufaa kwa adui.”
Aliachiliwa kutoka kwenye jeshi la Uingereza baada ya kukamatwa mapema mwaka huu na alikuwa amekanusha madai hayo. Kesi yake itatajwa Novemba.
Kutoroka kwake kumesababisha ukaguzi wa ziada wa usalama katika viwanja vya ndege na Bandari ya Dover, mashua kuu inayovuka kutoka Uingereza kwenda Ufaransa lakini shughuli ililenga Richmond Park, ekari 2,500 (hekta 1,000) za misitu na nyasi kama maili 5 (kilomita 8) kutoka Gereza la Wandsworth.