Polisi watatu kati ya zaidi ya Polisi kumi wa Mkoani Njombe waliokuwa kwenye gari la Polisi wamefariki Dunia katika ajali iliyotokea leo Feb 03, 2020 baada ya gari hilo la polisi kugongana na basi la abiria mali ya kampuni ya Sharon, RPC Njombe amethibitisha .
“Polisi watatu wamefariki na mwingine yupo mahututi tunafanya mpango wa kumsafirisha kwa ndege kwenda MOI, basi limeligonga gari la Polisi, Polisi wakarushwa, basi likapitiliza na kutaka kutumbukia Mtoni yangetokea maafa makubwa sana, ila wote kwenye basi wamepona” – Hamis Issa
BOSS MPYA ZIMAMOTO AONGEA KWA MARA YA KWANZA ANACHOENDA KUFANYA