Taarifa iliyonifikia Leo March 21 2016 kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum Dar es salaam Simon Sirro ni hili tukio la majambazi watatu kuuawa katika eneo la Masaki mwisho Dar es salaam.
Tukio lilikuwaje? Kamanda Sirro anasema ‘Mnamo tarehe 21 03 2016 majira ya saa 09:45, huko masaki mwisho watuhumiwa watatu wakiwa na gari namba T.125 BQJ RV4 Silver ,Bastola tatu na bomu la kurusha wakiwa kwenye harakati ya kumvamia mfanyabiashara mmoja aliyekuwa anapeleka fedha kwenye duka la kubadilishia fedha za kigeni‘- Simon Sirro
‘Askari walipata taarifa kutoka kwa raia wema, walifika haraka eneo latukio, ndipo wakakuta gari hiyo limepaki na kumwamuru jambazi aliyekuwa amebaki kwenye gari hilo afungue vioo na mtuhumiwa alikaidi amri hiyo na kufyatua risasi‘- Simon Sirro
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE