Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limewabadilisha kazi askari wake 164 wa kikosi cha usalama barabarani baada ya kubainika na vitendo vya rushwa.
Kamanda Suleimani Kova akizungumza mbele ya waandishi wa habari alisema>>
“Kwakuanza tumeamua hawa askari ambao wanalalamikiwa ambao ni wakaguzi 7 pamoja na askari wa vyeo mbalimbali wapatao 157 hao tumewatoa na wamebadilishwa kutoka kusimamia kazi za usalama barabarani na tumewapatia kazi za kawaida ” ;- Suleiman Kova
“kwamaana hiyo tumewateua wengine ili kuziba nafasi nafasi zao, pia makamanda wa polisi mikoa ya Ilala,Kinondoni na Temeke tumewapa maagizo kwamba waendelee kufuatilia mienendo ya askari wengine ili tuhakikishe wananchi wanapata huduma zilizo bora kutoka jeshi la polisi”;- Suleiman Kova
Iko hapa sauti ya kamanda wa Polisi Dar es salaam Suleiman Kova>>>
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE