Bondia maarufu nchini Kareem Mandonga aliyekwenda Kigoma kwa ajili ya pambano amelazimika kuahirisha safari yake ya ndege kurejea Dar es salaam leo baada ya uongozi wa Mkoa wa Kigoma kumpa dili nono la kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana Kigoma.
Mandonga amepata mwaliko wa kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Esther Mahawe na Katibu Tawa wa Mkoa huo ambapo Viongozi hao wamempongeza Bondia huyo kwa juhudi anazozionesha katika michezo yake.
Mandonga amesema anamshukuru sana Mungu kwa fursa aliyompatia ya kufahamika baada ya kupigwa na Bondia Shabani Kaoneka ambapo amesema Kaoneka ni kama amemfungulia njia ya kupata mafanikio katika maisha yake.