June 22 2016 Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Ilala limetoa tahadhari kupitia kwa Kamanda wa polisi mkoa Ilala, Salum Hamduni amesema hivi karibuni kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu (MATAPELI) kutumia vibaya majina ya viongozi wakubwa/mashuhuri wa serikali kwa kujipatia fedha/mali kinyume na utaratibu wa sheria za nchi.
Kamanda Hamduni amesema watu hao wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kuwatapeli watu wenye fedha kutoa kiasi cha fedha au mali wakiwatishia kwamba wasipo tekeleza maombi hayo watawajibishwa na viongozi hao.
Ameongeza pia mbinu wanazotumia watuhumiwa hao ni pamoja na kuwapigia simu za mikononi na za mezani (Land Line watu wenye fedha, wakijifanya kwamba wao ni viongozi wakubwa serikalini kama Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Aidha uchunguzi wa Jeshi hilo umebaini kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kwa kufungua akaunti bandia za viongozi hao mmoja ya akaunti iliyofunguliwa ni rc.poulmakonda.co.tz wakijifanya kuwa ni ya Mkuu wa Mkoa Dar Es salaa huku wakitumia kuwatapeli watu.
Watu hao pia wamekuwa wakitumia mbinu ya kuiga sauti ya viongozi hao wakiwataka watu wenye fedha watoe kiasi cha fedha au mali huku wakiwatishia wasipofanya hivyo watawachukulia hatua.
Jeshi la Polisi Mkoa ILala limefanikiwa kumkamata mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Imarock Paula Rutashobya @Issa Mohamed Jiunga kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu wa kutumia jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Mkaonda.
ULIKOSA MAMBO SITA YA GOODLUCK BAADA YA KUVULIWA KOFIA YA BARAGHASHIA BUNGENI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB INSTAGRAM YOUTUBE