Leo January 2, 2018 nikusogezee taarifa kutoka nchini Nigeria kwa President Muhammadu Buhari ambazo zinaeleza kuwa takribani watu 700 ambao walikuwa mateka wa kundi la waasi la Boko Haram wamefanikiwa kutoroka mikononi kwa kundi hilo.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Jeshi nchini humo Kanal Timothy Antigha amesema kuwa wamefanikiwa kutoroka kupitia visiwa kadhaa vya ziwa Chad na kufanikiwa kufika katika mji wa Monguno, katika jimbo la Borno.
Wakati akitoa salamu za Mwaka Mpya, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameeleza kuwa tangu mwaka 2009, Boko Haram wameua raia zaidi ya 20,000 huku mamilioni ya wengine wakitekwa na kupotea na kupotezana na familia zao.
Magari ya gharama yaliyonunuliwa na vijana mwaka 2017 Mwanza.
“Kuna mahali chama chetu tulikosea tukaacha kufanya mambo ya msingi” Katibu CCM