Imekuwa kawaida watu wengi kulalamikia vitendo vya wizi wa vifaa mbalimbali katika magari eneo la bandari ya Dar es Salaam hali iliyopelekea leo Serikali kutoa tamko rasmi juu ya mkakati unaoandaliwa ili kukomesha wizi huo.
Akizungumzia mkakati huo Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles John Tizeba amesema;- “..Wizi huu umepungua kwa kiasi kikubwa sana na kwa sababu tumehakikisha kwamba kasoro zilizo kwenye gari zinatambuliwa kabla gari halijatolewa melini.. Kama sasa kasoro nyingine itabainika baada ya gari lile ikuwa limeshashushwa kutoka melini tujue ni wapi kasoro hiyo imefanyikia na kwa hivyo mtu yule tutampata tuu.. kwa sababu mfumo unaeleweka..”
Kumsikiliza Naibu Waziri huyo bonyeza play hapa.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook