Baada ya agizo la Rais John Magufuli kuwataka watumishi wote waliopewa posho za kuhudhuria kilele cha mbio za Mwenge, Madereva na Wasaidizi wa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya mbalimbali nchini ambao walikuwa tayari wamefika Mkoani Simiyu kushiriki sherehe hizo wameeleza kuumizwa na agizo la kurejesha fedha za kujikimu ambazo kiasi walizitumia kwa shughuli husika.
Madereva na wasaidizi hao wamedai agizo hilo lilitolewa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli limewatengenezea tatizo la kiuchumi baada ya kuwafikia kwa kuchelewa huku baadhi yao wakidai kuwa hawana uwezo wa kurejesha fedha hizo kwasababu hawakuomba kufanya safari hizo bali ilikuwa sehemu ya kazi zao na kiasi cha fedha hizo walizitumia kama walivyokubaliwa na ofisi kuwawezesha kufika na kuishi katika eneo hilo.
>>>Sisi hatukuomba kuja Bariadi kwenye sherehe za Mbio za Mwenge wa Uhuru. Tuliambiwa kuja na tukapewa fedha ambazo tumezitumia kwa mujibu wa mahesabu ya matumizi tuliyoandikiwa kwa sababu ilibidi tule na kulala kwenye nyumba za wageni. Hapo sisi kosa letu liko wapi:- Dereva
>>>Ilinibidi nimlipe mwenye chumba gharama zote za siku 7 ambazo nilitarajiwa kuishi hapa kama nilivyotumwa kwasababu ya uhaba wa vyumba. Sasa naanzaje kumwambia mwenye hotel anirudishie pesa yangu yote ili nirejeshe ofisini?:- Msaidizi wa mkuu wa mkoa
Hata hivyo, wakati wasaidizi wa viongozi hao wakionesha kuvurugwa na agizo hilo ambalo wanasema limewaingiza hasara ambayo imetokana na kutumwa wafanye wajibu wao, baadhi ya wakuu wa mikoa tayari wameshaanza kurejesha fedha hizo.
Hivi karibuni Rais Magufuli aliagiza viongozi wote pamoja na wasaidizi wao waliokuwa wamepanga kuhudhuria sherehe za kuzimwa Mwenge Mkoani Simiyu zilizofanyika siku ya Ijumaa, wasitishe safari zao na waliochukua posho wazirejeshe.
ULIMISS KUONA UJENZI WA MALL MPYA ARUSHA? NIMEKUWEKEA HAPA