Serikali ya Zimbabwe imechukua uamuzi wa kuwafukuza kazi wauguzi wote walioshiriki katika mgomo wa nchi nzima ambao ulianza jumatatu ya April 16, 2018.
Taarifa kutoka kwa Makamu wa Rais nchini humo Constantino Chiwenga ilieleza kuwa wameamua kuwafukuza kazi wauguzi hao kutokana na usumbufu waliopata wagonjwa.
Taarifa hiyo ya Makamu wa Rais iliyotolewa jana iliiagiza Bodi ya Huduma za Afya kuwaajiri wauguzi wengine ambao wanaelimu ya uuguzi lakini hawajaajiriwa, pamoja na wauguzi ambao tayari wameshastaafu.
Wauguzi hao waligoma ili kushinikiza kulipwa pesa zao za posho na kupinga mfumo wa serikali wa kuwalipa mishahara kwa madaraja.
Maagizo ya Naibu Waziri Shonza Bungeni leo