Siku za hivi karibuni nchi ya Scotland imekamata headlines za kimataifa baada ya alama za miguu zinazotajwa kuwa adimu sana na mjusi mkubwa zaidi duniani (dinosaur) zimegungulika huko nchini humo.
Mabaki hayo ya kiumbe huyo ambaye anakadiriwa kuishi miaka milioni 170 yamegunduliwa kwenye matope katika kisiwa kimoja nchini humo kijulikanacho kama Skye.
Mijusi hiyo kwa kawaida walikuwa mpaka kufikia urefu wa mita 15 na walikuwa na uzito wa hadi tani 10.
Wajiolojia wameeleza kuwa kugundulika kwa mabaki hayo ni suala la muhimu kwa historia ya viumbe duniani.
Mbowe na Viongozi CHADEMA walivyofikishwa Mahakamani