Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire amezungumza na waandishi wa habari leo March 8, 2018 kuhusu kupatikana kwa Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi Tanzania Abdul Nondo ambae aliripoti mwenyewe kituo cha polisi cha Mafinga wilayani Mufindi.
Kamanda Bwire amesema jalada kwaajili ya uchunguzi limefunguliwa ili kuweza kufahamu ukweli kama alitekwa au lah. “Baada ya kumhoji Nondo alisema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana ambao walimtekeleza Wilaya ni Mufindi,”