Taarifa iliyotolewa leo April 26, 2018 siku ya Sherehe za Muungano na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira, imesema, wafungwa 585 wataachiwa huru kuanzia leo, wengine 2,734 wakipunguziwa kifungo na hivyo wataendelea kubaki gerezani hadi watakapomaliza sehemu ya kifungo kilichobaki.
Rais anatoa msamaha huo kwa mujibu wa ibara ya 45(1) (d) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Ni mategemeo ya Serikali kwamba watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa Taifa na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani,” taarifa hiyo imesema
Msamaha mwingine unahusu wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama vile ukimwi, kifua kikuu na saratani.
Jenerali Rwegasira amesema wafungwa hao ni lazima wathibitishwe na jopo la waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa au Mganga Mkuu wa Wilaya.
“Pia kuna wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili, na ulemavu huo uthibitishwe”
BREAKING: RAIS MAGUFULI ALIVYOIPANDISHA HADHI DODOMA KUWA JIJI