Leo February 18, 2018 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako amesema Serikali itagharamia shughuli za mazishi ya mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji NIT, Akwilina Maftah aliyeuawa kwa risasi Februari 16, 2018.
Prof. Ndalichako ameyasema hayo Leo mbele ya waandishi wa habari ambapo amethibitisha kuwa Akwilina alikuwa katika majukumu yake akiwa anapeleka barua yake ya mafunzo kwa vitendo Bagamoyo.
“Mafunzo yale kwa vitendo yalikuwa yanatarajiwa kuanza February 26, 2018 hivyo Kifo chake kimeleta simanzi kwa wananchi wote na Serikali kwa ujumla,”- Prof. Ndalichako
Prof. Ndalichako amesema kuwa Akwilina alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wa kike waliojipambanua kwa kujua umuhimu wa elimu , alihakikisha kwamba anasoma kwa bidii kwa manufaa yake na familia yake, lakini pia alikuwa mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu.
Maagizo ya Rais Magufuli kwa Vyombo vya Dola kwa Waliosababisha Akwilina Kupigwa Risasi