Katika muendelezo wa mabadiliko muhimu ndani ya sekta ya kifedha nchini Tanzania, NCBA Tanzania imetangaza programu yake ya kibenki na ya kisasa, NCBA Now.
Hatua hii inaashiria mabadiliko muhimu yaliyopelekea huduma kuboreshwa,na ufikiaji zaidi wa wateja wake.
Uzinduzi wa NCBA Now unaenda bega kwa bega na mafanikio ya kifedha ya kipekee kwa mwaka wa fedha ulioishia Desemba 31, 2023, ukithibitisha zaidi sifa ya NCBA Tanzania kama kinara katika huduma za kifedha na uvumbuzi wa kiteknolojia.
NCBA Sasa inawaletea mabadiliko ya kipekee katika huduma za kibenki kwa wateja wake. Hii ni huduma inayopatikana wakati wowote na mahali popote.Iwe kupitia *150*24#, au kupitia programu ya NCBA Now inayopatikana kwenye App Store au Play Store, wateja wa NCBA Tanzania wanaweza kufuatilia akaunti zao, na kupata huduma za kifedha kiganjani mwao, na kwa urahisi kwa kubonyeza tu.
Programu ya NCBA Now ina idadi kubwa ya suluhisho zinazolenga kusaidia shughuli za benki, na kuongeza urahisi kwa wateja. Programu hii inawezesha wateja kufuatilia akaunti kwa wakati halisi, na watumiaji wanapata ufikiaji wa aina mbalimbali.Aidha, programu hiyo inawezesha chaguzi mbalimbali za uhamishaji wa fedha, malipo ya bili, na kuwapa wateja mamlaka juu ya fedha zao.
NCBA Now inasimama kama programu kinara katika kufanikisha shughuli za haraka kwa wateja, katika sekta muhimu kama vile uzalishaji, mafuta, gesi, na usafirishaji.
Katika maeneo haya yenye kasi kubwa, wakati ni wa muhimu, na NCBA Now inahakikisha kwamba wateja wanaweza kufanya shughuli zao za kifedha kwa haraka na kwa ufanisi, hata wakati wakiendelea na ratiba zao.Iwe ni kusimamia mishahara kwa wafanyakazi , au kushughulikia malipo ya vifurushi katika sekta ya usafirishaji, NCBA Now ndio suluhisho la uhakika linaloendana na mahitaji ya sekta mbalimbali.
NCBA Now inawawezesha wateja wake kufanya kazi kwa ufanisi, inayopelekea kuongeza ukuaji na ushindani katika maeneo yao husika.
Zaidi ya hayo, NCBA Now, haipo Tanzania pekee, wigo wake ni mpana kupitia mipaka ya Kenya na hivi karibuni itapatikana Uganda, Rwanda, na Ivory Coast.Ukuaji huu unathibitisha dhamira ya NCBA ya kutoa suluhisho za kibenki za ubunifu, ambazo zinavuka mipaka, na kuwawezesha wateja wake.
Kupitia uwepo wake wa kikanda, NCBA inathibitisha nafasi yake kama taasisi kuu ya kifedha, inayoendesha ukuaji wa kiuchumi na ustawi ndani ya Afrika Mashariki.Kwa muhtasari, NCBA Now, inawakilisha maono ya NCBA, ya kutumia teknolojia kubadilisha matumizi ya huduma za kibenki, na kuwawezesha wateja wake kufikia malengo yao ya kifedha kwa urahisi.