Ukiisikia China na Sheria zake ni msumeno kweli, wakiandika hukumu yao kama ni kunyongwa basi hakuna huruma itakayokuokoa.. wamefanikiwa kuzuia vingi kutokana na Sheria zao kali walizopitisha kwenye nchi yao.
Dongguan ni mmoja ya miji ambayo inaongoza kuwa na viwanda vingi sana, ishu ya Serikali ya China kuingiza kampeni mtaani ya kamata kamata kwa kila mtu ambae anajihusisha na biashara ya kujiuza kumbe imeathiri sehemu kubwa sana ya mapato ambayo huwa yanakusanywa kila mwaka kwenye Jiji hilo.
Kwa hesabu ya haraka wanasema hasara ya kuzuia biashara hiyo kwa karibia mwaka mmoja ni Dola bil. 8 zimepotea, kuna Mahoteli makubwa ambayo walikuta yanaruhusu wasichana kujiuza yalifungwa, sehemu nyingine ni kama zilizokuwa zinatoa huduma za massage, kote kulifungwa kabisa !!
Haimaanishi biashara ndio imekwisha, yani kuna wateja na watoa huduma hiyo ambao wanafahamiana kabisa, Serikali imesimamia kila kitu mtaani lakini bado mambo yanaenda chinichini, jamaa mmoja akasema yeye ni shuhuda.. aliunganishwa na msichana anayejiuza, akalipia dola 160 baada ya kuhudumiwa kwa dakika 90.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.