Binti wa paul kimiti Prudencia metoa msaada wa mahitaji mbalimbali ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha Watoto wetu Tanzania kilichopo Mbezi jijini Dar es salaam ikiwa ni kumshukuru Mungu kwa kupata bahati ya kupewa tuzo ya kufanyakazi kwa bidii nchini uingereza na Marikia Elizabeth wa Uingereza mwaka jana.
Msaada huo wa vitu mbalimbali vya mahitaji ikiwemo madaftari, sukali, mikeka ya kukalia, biscuit, pipi, pampas za watoto, juisi, taulo za kike, miswaki, pesa za nunua mtungi mkubwa wa gasi na mafuta ya kupikia.
Prudencia amesema tuzo aliyopata pia ni ya pongezi ya ilikuwa kwaajili ya kufanya kazi vizuri katika kusaidia wenye uhitaji wa kuonewa nchini uingereza.
“Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akasaidia mwaka jana nilipata bahati ya kupewa tuzo na marikia Elizabeth wa uingereza kabla hajafariki hivyo nimeona nije kutoa msaada huu ikiwa ni kumshukuru Mungu”
Aidha amesema tuzo hiyo aliyopewa sio ya pongezi kwaajili yake pekee bali ni pongezi kwa watanzania wote na pongezi kwa taifa zima la Tanzania.
Hatahivyo amewataka watoto hao wa kituo cha Watoto wetu Tanzania waishi vizri kwa kupendana, wasaidiane kwani wote ni ndugu
“Hata ukimuona mwenzako anapata shida yoyote hata kwenye masomo umsaidie kwani watoto wote katika kituo hicho ni ndugu kwahiyo naombeni sana mpendane na kusaidiana”