Ripoti mbalimbali za kimichezo zinasema kuwa Paris Saint-Germain wamewasilisha dau la €50m kwa fowadi wa Atalanta Rasmus Højlund (20), na wanasubiri majibu ya timu hiyo ya Serie A.
Jarida moja la Ufaransa liliripoti wiki iliyopita kwamba PSG walikuwa wameanzisha mazungumzo ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark.
Majadiliano hayo sasa yametoa zabuni ya €50m.
Les Parisiens hawataki kwenda juu zaidi kwa fowadi huyo mwenye umri wa miaka 20 na wanasubiri majibu ya Atalanta.
Walakini, PSG sio chama pekee kinachovutiwa na mchezaji huyo kwani kwa mujibu wa The Athletic, Manchester United pia wamewasilisha ombi la kutaka kumnunua Højlund, ambaye alijiunga na Atalanta kwa €17m pekee kutoka Sturm Graz msimu uliopita wa joto. Dau la Mashetani Wekundu lina faida kubwa kuliko PSG.
Kwa mujibu wa ripoti ya The Athletic, ofa ya Manchester United ina thamani ya €50m pamoja na €10 katika bonasi.
Iwapo ombi la PSG litakataliwa, mabingwa hao wa Ligue 1 watalazimika kuendelea kutafuta namba tisa.