Kocha wa Paris Saint-Germain Luis Enrique alikuwa na matumaini kuwa timu yake bado ingetinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kushindwa kwa bao 1-0 ugenini na Borussia Dortmund katika mechi ya mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali Jumatano.
“Ni mpira wa miguu. Mara nyingi sana ni wa kustaajabisha na nyakati nyingine inakuwa hivi. Tungependelea kuwa katika hali tofauti, lakini nadhani unapoutazama ulikuwa mchezo sawa,” Mhispania huyo aliambia mtangazaji Canal Plus. baada ya timu yake kutenduliwa na bao pekee la Niclas Fuellkrug katika kipindi cha kwanza.
Mabingwa hao wa Ufaransa walikuwa na uwezo wa kumiliki mpira zaidi na majaribio mengi zaidi kwenye goli lakini walizuiwa na umaliziaji mbaya na pengine kukosa bahati — Kylian Mbappe na Achraf Hakimi waligonga nguzo tofauti katika hatua moja katika kipindi cha pili.
“Hakuna aliyewahi kusema itakuwa rahisi katika nusu-fainali ya Ligi ya Mabingwa. Vijana kwenye chumba cha kubadilishia nguo wako chini kidogo. Tulipata nafasi moja ambapo tuligonga nguzo zote mbili,” Luis Enrique aliongeza.
“Lazima useme huu ni uwanja wa kipekee lakini nina uhakika tutakuwa na nguvu sana mjini Paris na hatuna cha kupoteza.”
Ni mechi ya tano pekee kwa PSG kupoteza msimu mzima, na mara ya kwanza walichapwa chini ya Luis Enrique bila kufunga bao.