Kamishna wa Uhamiaji, Uraia na Passport, Gerald Kihinga amesema Mtanzania atakayepoteza hati ya kielektroniki ya kusafiria inayopatikana kwa Shilingi 150,000 atalazimika kulipa Shilingi 500,000 kupata mpya.
Pia aliongeza kuwa iwapo ataipoteza tena hiyo aliyoipata kwa Tsh. 500,000 basi atalipa Tsh. 750,000 ili aweze kupata nyingine.
Ameyasema hayo katika uzinduzi wa utoaji wa hati hizo ambapo tayari hati 15,101 zimeshatolewa kwa Watanzania tangu kuanza kwa utoaji huo January mwaka huu.
Kihinga amesema zipo kesi nyingi za watu kupoteza hati zao za kusafiria na baadhi yake ni zile zinazotokea katika matukio yasiyohitaji uwapo wake hati hizo hivyo gharama hiyo itasaidia watu kutunza hati zao.