Vladimir Putin alikuwa na mazungumzo ya simu na mkuu wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, leo asubuhi ambapo walijadili njia za kupunguza mzozo huko Gaza pamoja na juhudi za misaada ya kibinadamu, Kremlin ilisema.
Pia ilisema Bw Abbas alikubali kuzuru Urusi baadaye.
Urusi na rais wake wameunga mkono kwa nguvu Gaza na kupinga hatua ya kijeshi ya Israel katika eneo hilo – wakiunga mkono rasmi wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano katika Umoja wa Mataifa.
Putin pia aliishutumu Israeli kwa kutafakari mbinu zinazolingana na kuzingirwa kwa kikatili kwa Ujerumani ya Nazi huko Leningrad (sasa St Petersburg) katika Vita vya Pili vya Dunia.