Rais wa Urusi Vladimir Putin anazuru Kyrgyzstan kwa safari yake ya kwanza nje ya nchi tangu Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kutoa hati ya kukamatwa kwake kutokana na uhalifu wa kivita nchini Ukraine.
Bw Putin aliwasili katika taifa hilo la Asia ya kati siku ya Alhamisi kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili kwa ajili ya mikutano baina ya nchi hizo mbili na sherehe ya kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kambi ya kijeshi ya Urusi ya Kant nje ya Bishkek, mji mkuu wa Kyrgyzstan.
Mkuu huyo wa Kremlin amekuwa na safari mara chache nje ya nchi tangu aanzishe kile alichokiita “operesheni maalum ya kijeshi” nchini Ukraine mapema mwaka 2022 na haijulikani kuwa ameondoka Urusi tangu kibali cha ICC kutolewa.
Baadaye Putin anatarajiwa kusafiri hadi Uchina kwa kongamano la Beijing’s Belt and Road Initiative