Rais Putin amesema baadhi ya nchi “zinaendeleza ukoloni” ambao ulisababisha “mgogoro mkubwa” nchini Ukraine.
Amesema hayo akizungumza kwa njia ya video katika mkutano wa Brics unaofanyika nchini Afrika Kusini
Putin amesema hatua za Urusi nchini Ukraine ni kujibu vita “vilivyoachiliwa” na nchi za Magharibi. Anasema “matamanio” yao ya “kuhifadhi enzi zao duniani”, yalisababisha mapinduzi ya kijeshi nchini Ukraine (mwaka 2014).
Gavana wa eneo la Belgorod nchini Urusi alisema Jumatano kwamba raia watatu waliuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani katika kijiji kilicho karibu na mpaka wa Ukraine.
Akichapisha kwenye Telegram Vyacheslav Gladkov alisema: “Vikosi vya kijeshi vya Ukraine vilirusha kifaa cha kulipuka kupitia ndege isiyo na rubani wakati watu walikuwa mitaani.” Lavy ni takriban kilomita 21.51 (13.37 mi) kaskazini mwa mpaka wa Ukraine na Urusi. Ukraine bado haijatoa taarifa yoyote.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema ilizuia shambulio la ndege isiyo na rubani ya Ukraine dhidi ya Moscow usiku kucha.
Ilisema ndege zisizo na rubani mbili ziliangushwa na ulinzi wa anga; lakini meya wa jiji hilo alisema la tatu liligonga jengo lililokuwa likijengwa.
Safari za ndege katika viwanja vya ndege vitatu kuu vya Moscow – Sheremetyevo, Domodedovo na Vnukovo – zilisimamishwa kwa muda mfupi, kwa usiku wa pili.
Kyiv hajatoa maoni yake juu ya madai ya hivi karibuni