Rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwa amepanga kuuteka mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv ndani ya siku mbili, mkuu wa CIA William Burns amesema.
Akizungumza katika kikao cha bunge siku ya Jumanne, Burns aliwaonya wabunge wa Marekani: “Nadhani Putin amekasirika na amechanganyikiwa hivi sasa. Kuna uwezekano anaweza kujaribu kuwakandamiza wanajeshi wa Ukraine bila kujali majeruhi wa raia.”
Burns alisema Putin amekuwa “akisisitiza katika mchanganyiko wa malalamiko na matamanio kwa miaka mingi”.
Alielezea uvamizi wa Februari 24 wa Ukraine kama suala la “uaminifu wa kina wa kibinafsi” kwa kiongozi wa Kremlin.