Rais wa Urusi Vladimir Putin ametia saini msururu wa mikataba na mwenzake wa Vietnam To Lam wakati wa ziara ya kiserikali ambayo inakuja wakati Moscow inataka kuimarisha uhusiano barani Asia ili kumaliza kutengwa kwa kimataifa juu ya hatua zake za kijeshi nchini Ukraine.
Wawili hao walitia saini mikataba ya ushirikiano zaidi katika masuala ya elimu, sayansi na teknolojia, utafiti wa mafuta na gesi na afya.
Pia walikubali kufanya kazi kwenye ramani ya barabara kwa kituo cha sayansi na teknolojia ya nyuklia huko Vietnam.
Kufuatia mazungumzo hayo, Bw Putin alisema kuwa nchi hizo mbili zina nia ya “kukuza usanifu wa kuaminika wa usalama” katika Kanda ya Asia-Pasifiki kwa msingi wa kutotumia nguvu na kusuluhisha mizozo kwa amani bila nafasi ya “kambi zilizofungwa za kijeshi na kisiasa”.
Bw Putin alikuwa amewasili katika Ikulu ya Rais ya Vietnam siku ya Alhamisi alasiri, ambapo alilakiwa na watoto wa shule wakipeperusha bendera za Urusi na Vietnam.