Muhubiri mmoja wa kanisa la Seventh Day Adventist Nicolas Niyibikora huenda akajikuta anaingia katika matatizo na vyombo vya habari baada ya kuwaita wanawake ”chanzo cha uovu” katika mahubiri ya redio nchini Rwanda.
Niyibikora aliwaambia wanawake kwamba hawapendwi na Mungu wakati wakati akitoa matangazo ya idhaa ya redio ya Amazing Grace, January akionya kuwa ”hakuna lolote jema linaloweza kupatikana kutoka kwa wanawake”.
”Unaposoma Biblia , ni nani aliyeleta dhambi duniani”? Aliuliza akiongeze, ”sio mwanamume”.
Tayari mahubiri hayo yamewakasirisha wanaharakati huku wale wanaounga mkono usawa wa kijinsia wakiitisha mkutano na vyombo vya habari na kuonya kuwa maneneo kama hayo yanaweza kusababisha chuki na mzozo miongoni mwa raia wa Rwanda iwapo hakuna hatua ya haraka itachukuliwa.
Kundi la kutetea haki za wanawake liliwasilisha malalamishi yake katika tume ya udhibiti wa vyombo vya habari ambayo inatarajia kukutana ili kuzungunmzia kuhusu suala hilo wiki ijayo.
Afsa mkuu Emmanuel Mugisha aliambia gazeti la New Times kwamba kuna uwezekano idhaa hiyo italazimika kujieleza.
HAMISA MOBETTO KAFUNGUKA MAHAKAMA KUMSULUHISHA NA DIAMOND “UGOMVI WA FAMILIA UACHENI TU”, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA
ALICHOZUNGUMZA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KESI YAKE NA HAMISA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA