Usiku wa Septemba 15 2016 michuano ya Europa League ilichezwa barani Ulaya, klabu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilicheza dhidi ya Rapid Wien ya Austria na kufungwa goli 3-2, magoli mawili ya Genk yalifungwa na Leon Bailey.
Baada ya mchezo huo kumalizika Septemba 16 shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kupitia account yao rasmi ya twitter walitoa majina ya wachezaji 11 wanaounda timu bora ya wiki na kwa KRC Genk ametajwa mjamaica Leon Bailey, Bailey anaingia katika kikosi hicho kati ya zaidi ya wachezaji 528 waliocheza mechi za Europa jana.
Leon Bailey wa Genk ameingia katika kikosi bora cha wiki cha Europa League, Man United haijatoa mchezaji hata mmoja. pic.twitter.com/t4mS1h50mS
— millard ayo (@millardayo) September 16, 2016
Kwa upande wa kikosi bora cha UEFA Champions League wametajwa nyota kadhaa wakiwemo wa FC Barcelona lakini kwa upande wa Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Real Madrid hawakufanikiwa kutoa hata mchezaji mmoja katika kikosi hicho.
Kikosi bora cha wiki cha Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid haijatoa hata mchezaji mmoja pic.twitter.com/ZUI61Og7js
— millard ayo (@millardayo) September 16, 2016
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0