Qatar inapanga kuzinyakua klabu za Uhispania Malaga na Santos kutoka Brazil baada ya Sheikh Jassim kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kutwaa Manchester United.
Mfanyabiashara huyo wa Qatar alikuwa mmoja wa watangulizi wawili – pamoja na Sir Jim Ratcliffe – katika kinyang’anyiro cha kuchukua United, baada ya familia ya Glazer kufungua mchakato huo Novemba mwaka jana. Ratcliffe sasa yuko tayari kununua asilimia 25 ya hisa ya klabu – kwa mtazamo wa muda mrefu wa kuchukua kabisa Old Trafford.
Bodi ya United sasa itapiga kura kuidhinisha uwekezaji kutoka kwa Ratcliffe, tajiri mkubwa zaidi wa Uingereza, wiki hii hatua ambayo itamfanya awe mwanahisa mkubwa zaidi wa kilabu anapotarajia kuchukua udhibiti wa maamuzi ya michezo.
Hata hivyo, hatua inayofuata ya Sheikh Jassim bado haijulikani, ingawa uwekezaji kutoka Qatar katika vilabu vingine vya soka kuna uwezekano.
Rais wa Paris Saint-Germain Nasser Al-Khelaifi alihusika katika hatua ya Sheikh Jassim kuinunua United kwa kumshauri mfanyabiashara huyo kuhama.
Sheikh Jassim hajaunganishwa na kampuni ya Al-Khelaifi ya Qatar Sports Investments (QSI), ambayo kwa sasa inapanga kuwekeza katika vilabu vingine kadhaa vya kandanda, lakini wawili hao watakuwa na maslahi ya pamoja.