Qatar hatimaye imejitoa katika mazungumzo ya kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka kati ya Israel na Hamas, maafisa wanasema.
Nchi hiyo ilisema itaanza tena kazi yake wakati Hamas na Israel “zitaonesha nia ” ya kufanya mazungumzo.
Haya yanajiri baada ya maafisa wakuu wa Marekani kuripotiwa kusema kuwa Washington haitakubali tena kuwepo kwa wawakilishi wa Hamas nchini Qatar, wakishutumu kundi la Wapalestina kwa kukataa mapendekezo mapya ya kusitisha vita huko Gaza.
Qatar ilisema ripoti za awali kuwa ilijiondoa kwenye mazungumzo ya upatanishi na kusema kuwa ofisi ya kisiasa ya Hamas huko Doha “haifanyii kazi tena lengo lake” hazikuwa sahihi.
“Qatar iliziarifu pande hizo siku 10 zilizopita wakati wa majaribio ya mwisho ya kufikia makubaliano, kwamba itasimamisha juhudi zake za kupatanisha Hamas na Israel ikiwa makubaliano hayatafikiwa katika duru hiyo,” taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Qatar ilisema.