Rais wa Magufuli amewaagiza viongozi wa Manispaa ya Morogoro na viongozi wa Mkoa huo kuwaacha wafanyabiashara wadogo wadogo waendelee kufanya biashara zao katika eneo la Kituo Kikuu cha mabasi, Msamvu.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo July 27, 2017 baada ya msafara wake uliokuwa unatokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam kusimamishwa na wananchi eneo la Msamvu na kumueleza kero ya kunyanyaswa na Manispaa wakifukuzwa katika maeneo wanayofanyia biashara hasa baada kituo cha mabasi cha Msamvu kujengwa upya.
Mbali na hilo, Rais Magufuli amemuagiza RPC Morogoro SACP – Ulrich Onesphory Matei kuhakikisha Askari Mgambo hawawasumbui wafanyabiashara wadogo wadogo na kuwataka wafanyabiashara hao kutofanya vurugu wakati utaratibu mzuri unaandaliwa kwa ajili yao.
Aidha, Rais Magufuli amewataka watu waliobinafsishiwa viwanda mbalimbali mkoani Morogoro kuvirejesha Serikalini kama wameshindwa kuviendeleza ili wapewe wawekezaji wengine wenye uwezo wa kuviendeleza na kuzalisha ajira.
>>>”Ninarudia wito wangu nilioutoa nyuma, kwamba wenye viwanda hapa Morogoro ambao wameshindwa kuviendesha, akiwemo Mbunge wa hapa wa CCM ambaye alibinafsishiwa viwanda vingi, kama ameshindwa kuviendesha avirudishe ili tuwape watu wengine kwa sababu vijana hawa wanakosa ajira, nazungumza kwa uwazi kwa sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu.” – Rais Magufuli.
“Matatizo yaliyo kwenye uwezo wa Kiongozi na hakuyatatua, nalala mbele na huyo Kiongozi” – JPM