Maafisa wa serikali wametangaza Watu zaidi ya 37 wamefariki wakiwemo watoto watano wa familia moja, baada ya mafuriko kuikumba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mji mkuu wa Kinshasa kufuatia mvua kubwa iloyonyesha nchini humo.
Wengi wa waliofariki ni wakazi wa mitaa ya Mabanda ambapo nyumba nyingi zimeharibiwa na maji ya mafuriko na maporomoko ya ardhi.
Wakazi milioni kumi wa mji wa Kinshasa wanaishi katika makazi duni katika maeneo tambarare na miundombinu ya kuondoa maji taka pia ni duni
Waziri wa jimbo Afya na Jamii Dominique Weloli, amesema “Kumetokea si tu mafuriko bali pia maporomoko ya ardhi na nyumba kadha zimebomoka.”
MSIBA: MWANAMUZIKI MKONGWE WA DANSI AFARIKI DUNIA