Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara leo imetoa zuio la muda dhidi ya matumizi ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao (Online Content Regulation) ambazo matumizi yake yalipaswa kuanza rasmi Mei 5, 2018.
Taasisi zilizowasilisha maombi hayo mahakamani ni Legal and Human Rights Cente (LHRC), Tanzania Human Rights Defenders (THRD), Media Council of Tanzania (MCT), Jamii Media, Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) na Tanzania Editors Forum (TEF).
Taasisi hizo katika kesi ya msingi ya mapitio ya kanuni hizo imewashitaki Waziri wa Habari, Tanzania Communication Authority (TCRA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Katika maombi ya msingi taasisi hizo zinaiomba Mahakama Kuu kufanya mapitio ya kanuni hizo kwa kigezo kwamba Waziri ametumia nguvu ya kisheria nje ya mamlaka yake, na zinakiuka kanuni za usawa.
Pia sababu nyingine ni kanuni hizo zinapingana na haki ya kujieleza, haki ya kusikilizwa, na haki ya usiri.
Kesi ya msingi imepangwa kusikilizwa May 10, 2018.
“Watu wameshikwa pabaya, Polisi sio wapigadebe wa CCM” –Lucy Mayenga