Taarifa zilizotufikia kutoka nchini Kenya ni kwamba takribani watu 32 wameuawa na wengine kutojulikana walipo baada ya bwawa la Solai kupasuka na kusababisha maafa.
Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo na kusababisha watu na nyumba kusombwa na maji na kusababisha vifo hivyo na kuacha watu zaidi ya 2000 bila makazi.
Kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu, wengi kati ya waliokufa ni wanawake na watoto ambao wameganda kwenye matope, na watu 40 hadi sasa wamekwisha okolewa.
Nape baada ya Sugu kuachiwa ‘nakumbuka uliimba juu yangu’