Kampuni ya Quality Media Group Limited imeinunua kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited ambao ni wachapishaji wa gazeti la kila siku la Jambo Leo na ununuzi huo umeanza December 31 2015 na unatarajiwa kukamilika Februari 2016.
Kampuni ya Quality Media imedhamiria kuwekeza katika tasnia ya habari kwa kuongeza ufanisi katika utendaji wa gazeti la Jambo Leo na kuahidi kufikia mwisho wa robo ya kwanza ya mwaka 2016 kuongeza machapisho mengine ikiwa ni pamoja na gazeti la kiingereza la kila siku na gazeti toleo la wiki la Afrika Mashariki.
Mkurugenzi mtendaji wa Quality Group, Bw. Arif Sheikh amesema Kampuni ya Quality Group imejipanga kuhakikisha kuwa Jambo Media inakuwa chombo cha habari bora na cha kuaminika nchini Tanzania katika ukanda wote wa Afrika Mashariki.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utakayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.