Kutoka nchini Kenya, jana April 5, 2018 Mahakama nchini humo imemhukumu askari polisi mmoja kifungo cha miaka 15 jela baada ya kukutwa na hatia ya kuua.
Inaelezwa kuwa polisi huyo alimuua kijana mmoja ambaye alisadikika kuwa mwizi wa simu ya mkononi mnamo mwaka 2013.
Polisi huyo Titus Musila alipatikana na hatia hiyo ya kumpiga risasi tatu kichwani kijana Kenneth Mwangi aliyehisiwa kuwa ameiba simu, badala ya kumkamata.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa haki za binadamu, polisi nchini Kenya wamekuwa wakilaumiwa kufanya mauaji lakini wamekuwa hawachukuliwi hatua.
LIVE: Msemaji Mkuu wa Serikali anazungumza na waandishi