Basi dogo limeacha njia na kuanguka kwenye korongo katika Mlima Peru na kuua watalii wawili wa Kijerumani na kujeruhi wengine 12.
Taarifa ya ajali hiyo imetolewa na Shirika la Habari la Serikali la Andina ambapo imeeleza kuwa kati ya waliojeruhiwa 10 ni raia wa Ujerumani.
Saa 24 kabla ya ajali hiyo inaripotiwa kuwa ajali nyingine ilitokea baada ya basi dogo kudumbukia kwenye mto na kuua watu saba huku ikijeruhi wengine 23.
Inaripotiwa kuwa ajali zinazoua watalii zimekuwa zikitokea mara kwa mara ambapo inaelezwa kuwa mwezi November 2017, ajali nyingine iliyotokea katika mji wa Huancavelica na kuua watalii wa Kijerumani wanne.
Alichofanya Mbunge wa Monduli baada ya Kaya na Mifugo 1000 kuharibiwa na mvua