Kutoka nchini Sudan Kusini aliyekuwa Mkuu wa Majeshi Paul Malong ameanzisha vugu vugu jipya la kundi la waasi.
Hatua hii imekuja kipindi ambacho nchi hiyo imeanza kufanya mazungumzo mapya ya amani jijini Addis Ababa Ethiopia yanayolenga kufikia makubaliano ya kuachiliwa kwa Makamu wa Rais Riek Machar.
Machar amewekwa kizuizini nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa Malong kundi lake hilo la waasi litakuwa na kazi ya kurejesha demokrasia na maendeleo ambayo yamepotea nchini humo.
Malong anadai kuwa serikali ya sasa imekuwa makosa mengi ya rushwa na kuifilisi nchi hivyo anataka kubadili nchi hiyo.
Jionee Jengo refu kuliko yote ARUSHA na la kwanza TANZANIA la utalii