Watu takribani 50 wanaripotiwa kuuawa katika shambulio la gesi ya sumu huko Ghouta Mashariki weekend iliyopita huku baadhi ya watu wakidai kuwa waliouawa ni zaidi ya 150.
Inadaiwa kuwa shambulio hilo ambalo lilifanyika katika mji wa Douma lilitokea Jumamosi jioni mara baada ya kuanza mashambulizi yaliyofanywa na majeshi ya serikali ya Syria baada ya makubaliano ya kusimamisha mapigano kutofanikiwa.
Serikali ya Marekani imeitaka Urusi kuacha kuisaidia serikali ya Syria na kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa katika kuepusha, mashambulizi ya kinyama ya kutumia silaha za kemikali.
MRADI WA DMDP: ‘Maamuzi sahihi Uambatana na Twakimu sahihi’