Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Humprey Polepole leo April 18, 2018 amezungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya Mkaguzi mkuu wa serikali na kuzungumzia pia madai yanayozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Shilingi Trilioni 1.5 iliyotanjwa kwenye ripoti ya CAG.
Polepole amewaambia waandishi wa habari kuwa suala la pesa hiyo Trilion 1.5 kutojulikana zilipo kama anavyodai kiongozi wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ni ya uongo na kumweleza kuwa ifikapo mwaka 2020 Zitto atafute kazi nyingine kwani hatarudi bungeni.
Akijibu yaliyosemwa na Polepole, Zitto kabwe kwenye kurasa zake za twitter na fb ameandika ujumbe unaosema hivi
“Kuna mtu anasema nikamatwe kwa kupotosha Kuhusu TZS 1.5trn zinazohojiwa na CAG.” -Zitto Kabwe
“Mimi Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mwenyeji wa Kigoma, Muislam, NAAPA kwamba Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano imeshindwa kuonyesha kwa CAG matumizi ya shilingi trilioni MOJA na Bilioni MIA TANO.” -Zitto Kabwe
“Nipo tayari kukamatwa kwa kusema hivyo ( haitafuta ukweli wa ubadhirifu huo ). mawazo yangu hayatakufa.” -Zitto Kabwe
BREAKING: Polepole anazungumzia Ripoti ya CAG na mengine