Leo January2, 2018, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amefanya ziara ya kukagua magari ya polisi yaliyopo Bandarini. Baada ya ukaguzi amesema ataunda kamati ya wataalamu kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa magari yote ni baada ya kubaini kuwa baadhi ya magari yana hitilafu mbalimbali.
Mhandisi Masauni amesema “Nyote mnafahamu jinsi tulivyo na changamoto ya magari kote nchi, katika ziara yangu kuna mambo nimeyagundua, nimeyakagua magari, kati ya magari 53 kuna magari matano yana hitilafu.”
JESHI LA POLISI ARUSHA LIMEFANYA UKAGUZI WA MAGARI NA KUKUTANA NA MAKOSA HAYA