Kutoka nchini Misri leo April 11, 2018 watu 30 wamehukumiwa kifo na Mahakama ya Kijeshi kutokana na makosa ya mashambulizi dhidi ya makanisa ya Coptic.
Mwishoni mwa mwaka 2016 takribani watu 70 walikufa kutokana na shambulio la bomu lililofanyika katika kanisa kuu la ki-Coptic mjini Cairo mwishoni mwa mwaka 2016.
April 2017 makanisa ya Alexandria na Tanta pia yalilipuliwa katika tarehe hiyo hiyo ya shambulio la kanisa hilo la mjini Cairo.
Kundi la wanamgambo wa Kiislamu nchini humo tayari wameshakiri kuhusika na mashambulio hayo yote.
Tanzania yashika namba 10 kwa kunywa Pombe AFRIKA