Leo April 30, 2018 Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari atakuwa kiongozi wa kwanza kutoka barani Afrika kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump, ikulu ya White house tangu aingie madarakani mwaka 2016.
Buhari na Trump wanatarajiwa kukutana baadaye katika Ikulu ya Trump jijini Washington DC ili kufanya mazungumzo juu ya mambo mbalimbali.
Inaelezwa kuwa wapo marais wengine wa Afrika ambao wamewahi kukutana na Trump lakini hawakukutana naye nchini Marekani ikiwa ni pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Wamiliki wa Sober House walalamikia Wabunge