Kama utakuwa unakumbuka vizuri katika somo la sayansi shule ya msingi kuna kitu kilikuwa kinaitwa mashine tata yaani kwa maana yake kwa lugha rahisi ni kitu chochote chenye uwezo wa kurahisisha kazi. Basi stori ipo hivi kocha wa timu ya taifa ya Ecuador Gustavo Quinteros anauguza jeraha la mguu lakini aliendelea na kukinoa kikosi chake.
Kocha huyo raia wa Argentina aliumia mguu wake September 16 wakati alipokuwa akicheza mpira na rafiki zake, Gustavo Quinteros ambaye anatarajia kupona baada ya mwezi, amelazimika kuingia uwanjani na kundelea kufundisha huku akiwa anatumia usafiri maalumu ni kama baiskeli au vipikipiki vidogo. Gustavo Quinteros alipewa ruhusu ya kuendelea kuifundisha timu yake inayojiandaa na michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018.
Gustavo Quinteros ameingia na kifaa hicho ambacho kinakitenga kwa mbele na ametumia kitenga hicho kuweka clipboard yake ya kufundishia, Ecuador wanajiandaa na mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Argentina October 9 mchezo utakaopigwa mjini Buenos Aries Argentina, kabla ya siku nne baadae kucheza nyumbani dhidi ya Bolivia.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE