Bila shaka umewahi kusikia tafiti nyingi pamoja na wataalamu wa masuala ya afya wakieleza madhara ya ulaji wa vyakula vya mafuta mengi ikiwa ni pamoja na kuongezeka uzito, magonjwa ya shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na mengineyo.
Utafiti mpya ambao umefanywa na wanasayansi wa Chuo kikuu cha Adelaide, Australia wamegundua kuwa ulaji wa vyakula vya mafuta mengi na sukari bila kula matunda mengi, huweza kusababisha tatizo la kuchelewa kupata ujauzito kwa wanawake.
Utafiti huu ambao umefanyika kwa wanawake nchini Australia, New Zealand, Ireland na Uingereza wameeleza kuwa walibaini kuwa wanawake wanaotumia matunda mara tatu kwa mwezi, wanachukua kiwango cha nusu mwezi kwa wastani kushika mimba.
Hii ni tofauti na wanawake ambao hula matunda mara tatu au zaidi kwa siku ambao hushika mimba haraka zaidi.
Utafiri umeeleza kuwa wanawake wasiokula matunda kwa wingi wana hatari ya 12% ya kutokuwa na uwezo wa kushika mimba katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja ukilinganisha na 16% ya wanaokula chakula chenye mafuta mengi, mara nne au zaidi kwa wiki.
JPM alivyomwaga Sh Milioni 3 kwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza