Usiku wa January 21 2017 wawakilishi pekee wa ukanda wa Afrika Mashariki katika michuano ya mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON 2017, timu ya taifa ya Uganda ilitolewa rasmi katika michuano ya mataifa ya Afrika yanayoendelea nchini nchini Gabon.
Uganda wameaga mashindano hayo baada ya kukubali kipigo cha goli 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Misri katika mchezo wao wa pili wa Kundi D, Uganda wanaaga mashindano hayo na kuwa wanasubiria mchezo wao wa kukamilisha ratiba dhidi ya Mali, hawana uwezo wa kufuzu hatua ya robo fainali hata wakipata ushindi wa aina yoyote ile.
Msimamo wa Kundi D kwa sasa baada ya Uganda kupoteza mchezo wa pili dhidi ya Misri kwa goli 1-0 #AFCON2017 pic.twitter.com/nFzGXGkM16
— millard ayo (@millardayo) January 21, 2017
Abdallah El Said wa Misri ndio alihitimisha safari ya Uganda katika michuano ya AFCON 2017, baada ya kufunga goli dakika ya 89 kwa kutumia vyema assist iliyotolewa na Mohamed Salah, kwa mujibu wa rekodi Uganda ni dhaifu kwa Misri, kwani leo wanakuwa wamefungwa kwa mara ya 16 na mara ya mwisho Uganda kuifunga Misri ilikuwa 1965 katika michuano ya kama hiyo.
https://youtu.be/zvPfx_DisvU
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4