Usiku wa October 20 2016 klabu ya KRC Genk inayochezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ilishuka katika uwanja wake wa Luminus Arena kucheza mchezo wake wa tatu wa Europa League dhidi ya Athletic Bilbao ya Hispania.
KRC Genk ambao tayari walikuwa wanaongoza msimamo wa Kundi F kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli ya Genk yakifungwa na Jakub Brabec dakika ya 40 na Wilfred Ndindi dakika ya 83.
Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta aliingia dakika ya 56 kuchukua nafasi ya nahodha wao Thomas Buffel, kwa sasa Mbwana Samatta anakuwa kaichezea Genk katika Europa League hatua ya Makundi kwa jumla ya dakika 126, mechi ya kwanza alicheza kwa dakika 77, ya pili 15 na 34.
Msimamo wa Kundi F iliyopo timu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania @samatta77 pic.twitter.com/9G3RbqrWVW
— millard ayo (@millardayo) October 20, 2016
Matokeo ya mechi za Europa League pic.twitter.com/Y2tEJ7RPrM
— millard ayo (@millardayo) October 20, 2016
https://youtu.be/uy543ywNLKg
ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1